🔖 Latest Blog Posts

Showing 6 of 6 posts

KIKAO CHA WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOSOMA DARASA LA SITA

Tarehe 21/11/2025 mwalimu mkuu amefanya kikao Cha wazazi wa darasa la sita na kueleza mikakati mbalimbali ya kuinua Taaluma na kukuza ufaulu kwa darasa la sita
Katika kikao hicho mwalimu mkuu ameongelea mambo mbalimbali kama ifuayavyo

1.Kuwajali wanafunzi kwa kuwanunulia vifaa vya kujifunzia na sare za shule
2.Kuwafaatilia watoto wao maendeleo ya shule kwa kutumia mfumo wa matokeo unaoitwa mwanzugi.com
3.Kuwa karibu baina ya mzazi na Walimu ili kumuendeleza mwanafunzi

Pia wazazi wamekubaliana kuwa wanafunzi wa Darasa la sita wasifunge shule na wasome kwa wiki tatu wakati wa likizo

Pia Kuwanunulia wanafunzi vifaa vifuatavyo
1.counter book query 3 saba
2.Daftari za msomi saba kwa ajili ya majaribio
3.Kuchangia kiasi cha Tsh. 5,000/= kwa ajili ya mitihani na motisha kwa walimu watakaokuwa wanafundisha wakati wa likizo

Pia mwalimu mkuu amewaomba wazazi kuisemea vizuri shule ya Msingi mwanzugi ili iweze kutangazika vyema

Posted on November 22, 2025, 8:36 pm

KALENDA YA MASOMO MWAKA 2026

*Ufafanuzi wa Kalenda ya Masomo kwa Mwaka 2026 – Tanzania*

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na *Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia*, mwaka wa masomo 2026 kwa shule za awali, msingi na sekondari umegawanyika katika mihula miwili kama ifuatavyo:

*Muhula wa Kwanza (Muhula I):*
- *Unanza:* 13 Januari 2026
- *Likizo fupi:* 27 Machi – 07 Aprili 2026
- *Unafungwa rasmi:* 05 Juni 2026
- *Idadi ya siku za masomo:* 96

*Muhula wa Pili (Muhula II):*
- *Unanza:* 06 Julai 2026
- *Likizo fupi:* 04 – 13 Septemba 2026
- *Unafungwa rasmi:* 04 Desemba 2026
- *Idadi ya siku za masomo:* 98

*Jumla ya Siku za Masomo kwa Mwaka Mzima:*
- *194 siku*

*Maana yake:* Mwaka 2026 kutakuwa na vipindi viwili vya masomo vyenye likizo fupi katikati, na shule zinatarajiwa kufundisha kwa siku 194 jumla. Wazazi, walimu na wanafunzi wanashauriwa kufuata ratiba hii kwa ukamilifu ili kufanikisha malengo ya kitaaluma.

Posted on November 21, 2025, 6:26 pm

TANGAZO KWA WAZAZI/WALEZI

Wito wa mkutano mkuu wa Wazazi/Walezi

Posted on November 20, 2025, 10:07 am

ZOEZI LA UPIMAJI

Walimu wakitimiza wajibu wao kwa kuwapima wanafunzi uwezo wa kusoma na kurekodi alama zao walizozipata

Posted on November 20, 2025, 8:47 am

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA 2025

Angalia matokeo ya Mtihani wa Taifa wa darasa la saba 2025 Shule ya Msingi Mwanzugi.
Fungua File hilo hapo chini

Posted on November 11, 2025, 4:05 pm

MZAZI NA MLEZI

Unakaribishwa kwa heshima kubwa kuhudhuria sherehe ya kuhitimu Darasa la Saba.
Tukio: Sherehe ya Kuaga Darasa la Saba
Tarehe: Jumamosi, 11 Oktoba 2025
Muda: Kuanzia saa 5:00 asubuhi
Mahali: Ukumbi wa St. Joseph
Ni furaha yetu kubwa kushiriki nawe siku hii ya pekee. Tafadhali fika kwa wakati.
Karibu Sana!

Posted on October 9, 2025, 3:12 pm